Page 112 - Fasihi_Kisw_F5
P. 112
Fasihi ya Kiswahili kwa Shule za Sekondari
Tumaini twaliweka, kwenu nafasi maisha,
Hatuna hata mkeka, sema utakuja kwisha,
Leo kumbe mwasikika, ipo siku mtakwisha,
FOR ONLINE READING ONLY
Kwa nini mwatunyanyasa, wakati wote twaishi?
Kurunzi (Mbijima 2019: 33 - 34)
Maswali
(i) Ni dhamira zipi za kimaadili zinazopatikana katika shairi hili?
(ii) Ni maadili gani unayoyapata kutokana na shairi hili?
(iii) Ni imani zipi unazozipata kutoka katika shairi hili?
(iv) Kuna uhusiano gani kati ya maadili yaliyoelezwa katika shairi hili na
maadili ya jamii yako?
(v) Ni kwa namna gani maudhui ya shairi hili hayaendani na maadili ya
jamii yako?
(b) Chagua mashairi mawili kutoka katika diwani mbili teule, kisha husianisha
maadili yaliyomo na imani za jamii.
Ulinganisho wa maadili na imani katika tamthiliya
Tamthiliya husawiri mambo halisi yanayotokea katika jamii, aghalabu utanzu
huu umeweza kuonesha uhusiano uliopo kati ya maadili na imani za jamii husika.
Kupitia utanzu huu, wanajamii huweza kujifunza namna ya kuishi na watu wa
hali mbalimbali kwa kuzingatia misingi ya kiimani na kimaadili.
Shughuli ya 4.8
(a) Soma matini fupi ya tamthiliya ifuatayo, kisha jibu maswali yanayofuata.
Megno: Habari za asubuhi Mtendaji
Mtendaji kata: (Kwa hasira) hatutoi misaada hapa, ondoka!
Megno: Aliyekwambia nimekuja kuomba msaada ni nani?
Mtendaji kata: Kilichokuleta nini?
Megno: Msidharau watu jamani. Hatukupenda kuwa hivi.
Kitabu cha Mwanafunzi 101
Kidato cha Tano
23/06/2024 17:54
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 101 23/06/2024 17:54
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 101