Page 111 - Fasihi_Kisw_F5
P. 111
Fasihi ya Kiswahili kwa Shule za Sekondari
Mate silaha ya kwetu, nyenzo yetu kuitunza,
Hatuna hata viatu, kutembea kwanzo funza,
FOR ONLINE READING ONLY
Kwetu sisi ni matatu, maagizo twajifunza,
Kwa nini mwatunyanyasa, wakati wote twaishi?
Kumbikumbi nakutaja, kwa jina lako heshima,
Sina sifa kulitaja, hata kwa liyesimama,
Ufanyayo si ya tija, kuishi kama mnyama,
Kwa nini mwatunyanyasa, wakati wote twaishi?
Muanzapo ota mbawa, nguvu mwajitangazia,
Mwatishia na vipawa, Mungu alo wajalia,
Mwaondoka kama njiwa, bila hata chungulia,
Kwa nini mwatunyanyasa, wakati wote twaishi?
Mwajifunza nyenyekevu, pindi tuko wote hapa,
Mwonesha wenu welevu, kumbe ziro tena kapa,
Hamna wenu welevu, ninyi kama hilo pipa,
Kwa nini mwatunyanyasa, wakati wote twaishi?
Leo ngoja tuyaseme, yenu haya ni maovu,
Tusije kuwa na shibe, kumbe ngozi ni makovu,
Badilika usisite, usije juta makovu,
Kwa nini mwatunyanyasa, wakati wote twaishi?
100 Kitabu cha Mwanafunzi
Kidato cha Tano
23/06/2024 17:54
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 100 23/06/2024 17:54
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 100