Page 109 - Fasihi_Kisw_F5
P. 109
Fasihi ya Kiswahili kwa Shule za Sekondari
kijana tu akatoweka. Alifahamu kuwa baba yake mdogo
atatuandikia. (Anaita tena). Huka...Nikija huko, kweli
nitakuchapa. Afadhali uje mwenyewe.
Huka (Ngahyoma, 1973)
FOR ONLINE READING ONLY
Maswali
(i) Ni dhamira zipi zinazopatikana katika matini hii?
(ii) Ni kwa namna gani matukio katika matini hii yanafumbata maadili?
(iii) Matendo ya wahusika yanasawiri maadili? Kwa nini?
(iv) Ni kwa namna gani lugha iliyotumiwa na wahusika inaakisi maadili?
(toa sababu)
(v) Ni matukio gani katika matini hii hayaakisi maadili ya jamii yako?
(b) Chambua maadili yanayopatikana katika tamthiliya mbili teule ulizosoma.
(c) Angalia au sikiliza tamthiliya mbili zinazorushwa katika vituo vya runinga
au redio, kisha chambua maadili yanayopatikana katika tamthiliya hizo.
Shughuli ya 4.5
Kwa kutumia vyanzo mbalimbali, chambua kazi nne za ushairi na nne za
tamthiliya, kisha bainisha masuala ya kiimani yaliyomo katika kazi hizo.
Ulinganisho wa maadili yaliyomo katika kazi za fasihi na imani za
jamii
Imani ni hali ya mtu kukubali jambo fulani kuwa ni kweli na anapaswa
kuliheshimu. Aghalabu, imani hujielekeza katika masuala ya dini. Miongoni
mwa maudhui yanayowasilishwa kwenye kazi za fasihi hutokana na imani
iliyomo katika jamii. Hivyo kuna uhusiano mkubwa baina ya maadili na imani.
Dhana hizi hujengana na kuathiriana kiasi kwamba wakati mwingine ni vigumu
kuvitenganisha. Ieleweke kuwa wakati mwingine kuna imani ambazo huweza
kumsukuma au kumwelekeza mtu kufanya matendo yasiyo na maadili. Kutokana
na uwasilishwaji wa masuala mbalimbali, ni muhimu kuzingatia imani za jamii
husika katika uchambuzi wa maadili yanayojitokeza katika kazi za kifasihi.
Ulinganisho wa maadili katika imani unaweza kuangaliwa katika kazi za kifasihi
kama vile bongo fleva, mashairi na tamthiliya.
98 Kitabu cha Mwanafunzi
Kidato cha Tano
23/06/2024 17:54
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 98
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 98 23/06/2024 17:54