Page 120 - Fasihi_Kisw_F5
P. 120
Fasihi ya Kiswahili kwa Shule za Sekondari
Jamani muogopeni, huyu si wa kutaniya
Usifanye ya utani, atakutia pabaya
Kidhabu toka zamani, hana kheri nakwambiya
FOR ONLINE READING ONLY
Mtesi mtu mbaya, hatari kuwa kundini
Ujiondowe kundini, makazi yako hawiya
Humo hutoonekani, pokea yako hidaya
Kama ukifanywa kuni, hiyari yake Jaliya
Mtesi mtu mbaya, hatari kuwa kundini
Umejitia shimoni, sasa unapayapaya
Kazi hiyo kwa yakini, umetafuta javiya
Japo upo walakini, jiepushe na hatiya
Mtesi mtu mbaya, hatari kuwa kundini
Adili za Nyembe 1: Tungo za Ustadh Mohamed Ally Nyembe (Akhery) (Ndossa
na Wenzake, 2019:5)
Maswali
(i) Mshairi anaibua mitazamo gani katika shairi hili?
(ii) Je, mitazamo iliyotolewa katika shairi hili inahusiana vipi na matendo
ya jamii?
(iii) Je, shairi lina mtazamo gani kuhusu madhara ya utesi?
(iv) Je mstari unaosema “Kama ukifanywa kuni hiyari yake Jaliya”
unawakilisha mtazamo gani?
(v) Je, mitazamo ipi katika shairi hili haiendani na matendo yaliyomo
katika jamii? Kwa nini?
Kitabu cha Mwanafunzi 109
Kidato cha Tano
23/06/2024 17:54
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 109 23/06/2024 17:54
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 109