Page 125 - Fasihi_Kisw_F5
P. 125
Fasihi ya Kiswahili kwa Shule za Sekondari
Avita: Usiniambie!
Vera: Ndo nakwambia sasa. Isitoshe, wasomi wengi wana migogoro
isiyo na suluhu ya ndoa. Wake zao wasomi wana mambo hamsini
kidogo. Mara wanaandika paper, mara vikao, mara appointment za
FOR ONLINE READING ONLY
mheshimiwa. Kwa kupenda au kutokupenda, kujua au kutokujua,
wanajikuta wanawaacha wanaume zao wakiwa na njaa, hapo ndo
wanatuachia njia nyeupeee. Kufa kufaana.
Avita: [Anaangua kicheko cha nguvu]. Yaani wewe umepinda, hapo ndo
nakupendea mtu wangu.
Beti: Yaani mnavunja ndoa za watu halafu mnapongezana? Mh!
Wonders will never end
[Anapiga makofi na kubetua mdomo kuonesha mshangao]
Vera: Point of correction, hatuvunji, kimsingi tunawasaidia kuondoa
stress zao.
Wakiingia kwenye mihadhara wapoleee. Fikiria wangekuja na
stress kwenye kumbi za mihadhara, si ingekuwa kimbembe.
Yaani, watu kama sisi ni wa muhimu kwa maendeleo ya taifa.
Beti: Nawahurumia, hamjui mlifanyalo, halafu mnaongea kwa sauti na
kujiamini. Akina mama wakitokea hapa, hamwogopi?
Halahala (Mbijima, 2019: 52 - 53)
Maswali
(i) Imani na mitazamo gani inajitokeza katika matini hii?
(ii) Mitazamo ya mwandishi kuhusu mwanamke ina athari gani katika
jamii?
(iii) “Nina wengine, siyo mwingine. Kwa uzuri huu wanaonitaka ni wengi,
lazima nibadili ladha.” Kauli hii inaweza kuleta athari gani kwa vijana?
(iv) Unafikiri mitazamo iliyomo katika matini hii ina uhalisi wowote katika
jamii? Kwa nini?
114 Kitabu cha Mwanafunzi
Kidato cha Tano
23/06/2024 17:54
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 114
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 114 23/06/2024 17:54