Page 97 - Fasihi_Kisw_F5
P. 97
Fasihi ya Kiswahili kwa Shule za Sekondari
Ben peke yake ndiye aliyekuwa na mimi. Jamaa za mume
wangu vilevile, walimtenga siku hiyohiyo ya ndoa. Lakini
nikaona si kitu tutaishi. Mimi, wewe, Herbert. Kwa nini
isiwezekane ikiwa pendo lipo? Kwa nini tusiweze? Lakini
FOR ONLINE READING ONLY
hata hi…
Chris: Ma!
(Kimya, Mtu anagonga mlango)
Martha: Mtazame nani.
(Ingia George)
George: Habari Martha.
(Martha hajibu)
A-a! Chris
(Chris hajibu. Baada ya muda)
George: Nimekuja kuchukua hati.
Martha: Hati?
George: Tunataka kuchukua maiti kutoka hospitali.
(Kimya)
Martha: Sina hati. Sisi tutamzika hapa. Nimeshamwomba Pasta
atatusaidia kumzika. Tumewaambia marafiki zetu watakuja.
Na wewe…
George: Utamzika wapi?
Martha: Hapa! Pale.
(Anaonesha nje ya dirisha)
George:: Ndivyo alivyousia marehemu?
Martha: Ndiyo.
George: Hakikisha.
Martha: Usinifokee. Kama unataka kufoka nenda nyumbani kwako.
86 Kitabu cha Mwanafunzi
Kidato cha Tano
23/06/2024 17:54
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 86
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 86 23/06/2024 17:54