Page 92 - Fasihi_Kisw_F5
P. 92
Fasihi ya Kiswahili kwa Shule za Sekondari
Shughuli ya 3.15
(a) Hakiki mashairi mawili kutoka katika diwani teule kwa kutumia nadharia
ya umuundo.
FOR ONLINE READING ONLY
(b) Soma shairi lifuatalo, kisha hakiki kwa kutumia nadharia ya ufeministi kwa
kujibu maswali yafuatayo.
Maisha ya Ndoa
Mume
Nimeagiza chakula, wanisogezea uji,
Nikiangalia saa, ni mwanana adhuhuri,
Ni ya msosi majira, umenitengea nini?
Haya maisha ya ndoa, wenzangu mnaishije?
Mke
Mboga unga na mkaa, mwenzangu mi’ sivioni,
Nimechoka kulalama, mapenzio siyaoni?
Unazicheza karata, pesa zako sizioni,
Haya maisha ya ndoa, wenzangu mnaishije?
Mume
Wewe mke sikiliza, tena usiwe shubiri,
Makonzi nitakutia, mke gani we bilisi!
Umepuya huna uja, hatari bora ya chui,
Haya maisha ya ndoa, mwenzangu mnaishije?
Mke
Mume tega masikia, nisikize kwa makini,
Majukumu nayajua, jikoni hadi chumbani,
Kuchapana zilipendwa, ndoa sio utumwani,
Haya maisha ya ndoa, wenzangu mnaishije?
Kitabu cha Mwanafunzi 81
Kidato cha Tano
23/06/2024 17:54
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 81 23/06/2024 17:54
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 81