Page 79 - Fasihi_Kisw_F5
P. 79
Fasihi ya Kiswahili kwa Shule za Sekondari
3. “Fani na maudhui ni kama pande mbili za sarafu.” Jadili kauli hii.
4. Eleza ubora na udhaifu wa mitazamo ya kidhanifu na kiyakinifu katika
kutoa maana ya fani na maudhui.
FOR ONLINE READING ONLY
Nadharia za uhakiki wa kazi za fasihi
Shughuli ya 3.4
Kwa kutumia vyanzo vya mtandaoni na maktabani, eleza maana, sifa na umuhimu
wa nadharia za uhakiki.
Dhana ya nadharia na nadharia ya uhakiki
Wataalamu mbalimbali kama vile Massamba na wenzake (2009) na Mulokozi
(2017) wanakubaliana kuwa nadharia ni utaratibu au mwongozo unaosaidia
kueleza jambo fulani. Kwa msingi wa fasili hii, nadharia ya uhakiki ni mwongozo
unaoelekeza namna ya kufafanua vipengele vya fani na maudhui ya kazi za fasihi.
Kwa muktadha wa kifasihi, Wafula na Njogu (2013) wanasema kwamba nadharia
za uhakiki ni miongozo inayomwelekeza msomaji wa kazi ya fasihi kuifahamu
kazi hiyo na vipengele vyake. Hivyo, nadharia za uhakiki wa kazi za fasihi ni
mawazo, maelezo au miongozo iliyopangwa ili kusaidia kufafanua vipengele
mbalimbali vya kazi hizo.
Sifa za nadharia za uhakiki wa kazi za fasihi
Nadharia za uhakiki huwa na sifa zifuatazo:
(i) kuwa na malengo mahususi yanayokusudiwa kutimizwa;
(ii) kuwa na misingi mikuu ambayo ni mwongozo wa uchambuzi au uhakiki; na
(iii) kuwa na mpangilio inayojengana na kukamilishana katika kufafanua mambo
yanayopatikana katika kazi husika.
Umuhimu wa nadharia za uhakiki wa kazi za fasihi
Nadharia za uhakiki zina umuhimu ufuatao:
(i) kumwongoza mhakiki katika uchambuzi na uhakiki wa kazi za fasihi kupitia
misingi na maudhui yake makuu;
(ii) kumsaidia mhakiki kuzielewa na kuzitumia nadharia mbalimbali za fasihi;
na
68 Kitabu cha Mwanafunzi
Kidato cha Tano
23/06/2024 17:54
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 68
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 68 23/06/2024 17:54