Page 136 - Fasihi_Kisw_F5
P. 136
Fasihi ya Kiswahili kwa Shule za Sekondari
madhara hutokea duniani kutokana na uongo wa watu wakubwa kuliko
ule wa watu wadogo. Ukitaka kuwa mwongo lazima usiwe msahaulifu.
Kutosahau ni jambo lifikirikalo lakini haliwezekani. Kwa hivi, njia ya
mwongo fupi. Uongo ni kama giza, hukimbia mbele ya cheche ndogo ya
FOR ONLINE READING ONLY
nuru ya kweli. “Uongo hukimbia kweli ikidhihiri” ni methali ya Kiswahili
ikumbushayo watu udhaifu wa uongo. Uovu mkubwa wa uongo ni mtu
kujidanganya mwenyewe. Jambo kama hili hutokea mara kwa mara kwa
waongo. Muongo humcha mno mtu kuliko Mungu.
Insha na Mashairi (Robert, 1967:1)
Maswali
(i) Ni maana zipi zinapatikana katika sentensi isemayo “Bahari moja ya
hatari katika dunia ni uongo”?
(ii) Msemo wa “Ukitaka kuwa mwongo lazima usiwe msahaulifu” una
maana zipi?
(iii) “Tashibiha” iliyotumika katika insha hii ina maana gani?
(iv) Ni maana zipi unaweza kuzipata katika sentensi ya “Baadhi ya madhara
hutokea duniani kutokana na uongo wa watu wakubwa kuliko ule wa
watu wadogo”?
(v) Ni taswira zipi unaweza kuziibua kutoka katika insha hii?
(vi) Ni maana zipi unaweza kuziibua kutokana na insha hii? Kwa nini?
(b) Soma insha ifuatayo, kisha chambua maana mbalimbali zinazopatikana
katika insha hiyo.
URAFIKI WA PAKA
Wanyama katika kuimarisha maisha yao, hujenga mahusiano wao kwa wao
na kwa binadamu. Binadamu huwatumia wanyama hawa kwa shughuli kadha
wa kadha. Wanyama wengine wana jukumu la kuleta burudani kwa binadamu
kama vile gwaride, nyimbo, ngoma na vichekesho. Paka ni mmoja wa wanyama
wenye urafiki na binadamu kutokana na mwenendo wake. Binadamu amekuwa
akimwamini na kumpa kiti cha kushughulikia mambo mengi ofisini mwake.
Sauti isikikayo mithili ya kinanda humpatia paka upekee wa ajabu. Akimwona
mgeni huimba kwa sauti nyororo! Nyau! Nyaau! Nyaaau! Nyaaaau! Mlio wake
Kitabu cha Mwanafunzi 125
Kidato cha Tano
23/06/2024 17:54
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 125 23/06/2024 17:54
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 125