Page 138 - Fasihi_Kisw_F5
P. 138
Fasihi ya Kiswahili kwa Shule za Sekondari
hunoa mikuki yake tayari kwa mawindo na maadui. Wakati wa burudani hufanya
mazoezi ya kupanda juu ya miti mirefu.
Ninawashauri watu wasiwapige paka kwa mawe; badala yake, wawajali na
kuwapatia mahitaji yao kama vile: chakula, maziwa, nyama na maji. Paka ni
FOR ONLINE READING ONLY
mfalme kwa watu wenye busara ya kujali viumbe. Urafiki wa binadamu na paka
unapaswa kuwa wa kudumu. Wanyama wengine hawana budi kuiga matendo ya
paka ili kudumisha urafiki na binadamu.
Shughuli ya 5.6
(a) Soma shairi lifuatalo, kisha jibu maswali yanayofuata.
Kifo cha Mende Wekundu
Na ujenge yako nyumba, jingi jasho likuoshe,
Ufyeke, upime na uweke nguzo,
Kisha paa na uweke na ukandike,
Siku nyingi bila kuingiliwa na mgeni hutakaa.
Wataanza kutalii mipaka mende usiku,
Nje na ndani ya nyumba watazunguka,
Bila woga, bila ruhusa ulichonacho watakula,
Masalia yatakuwa yako, ijara ya kaziyo.
Na nyingi dawa uweke, nyumba nzima uihame,
Ukae nje nzima siku usubiri,
Wazima wamelala ukirudi usiku,
Vichwa ngumu hawafi mende rahisi.
Kifo cha mende sharti miguu juu,
Kichwa ukikanyage kipasuke usikie,
Na kisha wengine usiku mchana uwasake,
Mpaka watakapokwisha. Usiseme nao.
Karibu Ndani (Kezilahabi, 1988:33)
Kitabu cha Mwanafunzi 127
Kidato cha Tano
23/06/2024 17:54
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 127 23/06/2024 17:54
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 127