Page 139 - Fasihi_Kisw_F5
P. 139
Fasihi ya Kiswahili kwa Shule za Sekondari
Maswali
(i) Ni maana zipi unaweza kuzipata katika mstari usemao “Wataanza
kutalii mipaka mende usiku”?
FOR ONLINE READING ONLY
(ii) Ni taswira zipi unaweza kuzijenga kutokana na jina la shairi hili?
(iii) Mstari usemao “Bila woga, bila ruhusa ulichonacho watakula” una
maana zipi?
(iv) Mstari usemao “Kifo cha mende sharti miguu juu” unamaanisha nini?
(v) Ni njia zipi umezitumia katika kupata maana za mistari iliyodondolewa
katika maswali namba i, iii na iv?
(vi) Ni maana zipi unaweza kuibua kutokana na shairi hili? Kwa nini?
(c) Soma mashairi mawili kutoka katika diwani teule, kisha, kwa uthibitisho wa
mifano, chambua maana na mbinu mbalimbali za kiujumi zinazopatikana
katika mashairi hayo.
Maana zinazopatikana katika tamthiliya
Shughuli ya 5.7
(a) Soma matini fupi ya tamthiliya ifuatayo, kisha jibu maswali yanayofuata.
Bi Moja: Vipi habari ya safari. Mbona umerudi na vitambaa vyote?
Bi Tano: Hakuna wanunuzi.
Wote: Aah hata! Haiwezekani!
Bi Moja: Hata haiwezekani! Sema tu hukwenda.
Bi Tano: [Amekasirika]: Yaani mnasema mimi mvivu siyo?
Nimezunguka mji mzima na zigo hilo halafu mnaniambia
mimi mvivu? Nawaambia watu hawataki kununua. Au mlitaka
niwagawie bure.
Bi Nne: Lakini kwa nini wakatae kununua hivi, mbona vile vya mwanzo
walinunua?
Bi Moja: Tena walikuwa wanavigombania.
128 Kitabu cha Mwanafunzi
Kidato cha Tano
23/06/2024 17:54
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 128
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 128 23/06/2024 17:54