Page 144 - Fasihi_Kisw_F5
P. 144
Fasihi ya Kiswahili kwa Shule za Sekondari
Shughuli ya 5.10
Kwa kutumia vyanzo vya mtandao, maktaba au matukio halisi, kusanya
mazungumzo ya makundi mawili (mtoto au watoto wadogo wenye umri wa
kuanza shule na kiongozi yeyote wa serikali kisha tathmini aina, maana na
FOR ONLINE READING ONLY
mpangilio wa hoja zinazotolewa katika mazungumzo ya kila kundi.
Misingi ya ujenzi wa hoja zenye mantiki na ushawishi
Ujenzi wa hoja zenye mantiki na ushawishi humtaka mtoahoja awe razini na
makini. Hoja hizo hujengwa kwa kuzingatia misingi ya uadilifu, ushawishi,
kudhihirisha uhakika wa jambo, hadhira, muundo, na mpangilio wa kimantiki.
Kwa muktadha wa ujenzi wa hoja, dhana ya uadilifu hujumuisha hali za ukweli,
usawa, heshima, usahihi, na uhalisi wa jambo linalowasilishwa. Mjengahoja
hutakiwa kuepuka kuwasilisha jambo kwa namna ya kumshambulia au kumbeza
mtu. Pia, hutakiwa kuwasilisha jambo lenye ukweli na la usahihi. Atumie data
sahihi ili kuipa nguvu hoja yake. Hivyo, hadhira yake itavutiwa na kuamini hoja
zake.
Mjengahoja pia hutakiwa kuwasilisha hoja zake kwa ufasaha. Aoneshe kujiamini
ili aiaminishe hadhira yake kuwa ana uhakika na anachokiwasilisha. Katika
maelezo ya hoja yake, aoneshe ufundi wa kuhusisha mifano na mazingira
halisi. Kwa kufanya hivi, huonesha mamlaka ya kimaarifa na kiujuzi juu ya
anachokiwasilisha; na hadhira hupata imani kuwa inapokea hoja kutoka kwa mtu
sahihi.
Pia, mjengahoja hutakiwa kutumia mbinu ya ushawishi kwa hadhira yake juu
ya kinachowasilishwa. Mjenzi mzuri wa hoja huzingatia suala la kugusa hisi za
hadhira yake ili kuihamasisha kupokea, kuamini na kutumia hoja zake. Nguvu ya
ushawishi husaidia kuimarisha kile kilichomo katika akili ya hadhira. Pia, kama
hadhira ilikuwa katika uelekeo tofauti wa jambo linalowasilishwa, ushawishi
husaidia kuivutia kwenye uelekeo wa mwasilishaji. Mbinu za kujenga ushawishi
ni pamoja na kutumia mifano halisi, mbazi, simulizi fupi, uteuzi wa maneno
yenye uwezo wa kuamsha hisia za hadhira, na semi mbalimbali kama vile
misemo, methali, nahau na misimu.
Kadhalika, mjengahoja anapaswa kuzingatia hali ya hadhira. Hali ya hadhira
hujumuisha uwezo wa kuelewa, wastani wa kiwango cha elimu, wastani wa
tajiriba ya maisha, mwelekeo wa malengo, matarajio, utamaduni, pamoja na
hali ya kisaikolojia. Uzingatizi wa hali hizo za hadhira humsaidia mjenga hoja
Kitabu cha Mwanafunzi 133
Kidato cha Tano
23/06/2024 17:54
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 133 23/06/2024 17:54
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 133