Page 145 - Fasihi_Kisw_F5
P. 145
Fasihi ya Kiswahili kwa Shule za Sekondari
kuteua na kutumia maneno, vipamba-lugha (kama vile toni na kidatu), na mifano
muafaka. Vilevile, humsaidia kutathimini uelewekaji wa wasilisho wakati
anaendelea kujenga hoja.
Isitoshe, mjengahoja anapaswa kuzingatia muundo mzuri. Mjenzi mzuri wa
FOR ONLINE READING ONLY
hoja lazima atafakari suala hili ambalo lina athari kubwa katika mpangilio wa
anachowasilisha. Hata kama hoja yake ni moja, lazima aiunde vyema. Ajiulize
kuhusu nini kianze kuwasilishwa na nini kifuatie. Kama hoja zipo zaidi ya moja,
atafakari kuhusu kubebana, kusababishana na kuendelezana kwa hoja hizo.
Hivyo, ni vyema aliunde wasilisho lake katika namna inayorahisisha kueleweka
kwake.
Kutathmini kazi za fasihi kwa kutumia misingi ya ujenzi wa hoja
zenye mantiki na ushawishi
Misingi ya ujenzi wa hoja zenye mantiki na ushawishi hutumiwa pia kutathmini
vipengele mbalimbali vya fani na maudhui katika kazi za fasihi. Misingi ambayo
hutumika kujenga hoja zenye mantiki na ushawishi ni pamoja na uadilifu,
ushawishi, kudhihirisha mamlaka, na kutilia maanani hadhira na muundo.
Miongoni mwa vipengele vilivyomo katika kazi ya fasihi ambavyo huweza
kutathminiwa ni matendo ya wahusika ambayo yakisawiriwa vyema hudhihirisha
hoja zenye mantiki.
Shughuli ya 5.11
(a) Kwa kutumia kipande kifuatacho cha tamthiliya, jenga hoja zenye mantiki
na ushawishi kuhusu ujenzi wa wahusika.
Mlinzi I: We, we … simama! (Anamkaribia Mwari I)
Nasema simama … nani aliyekutieni msuko huu?
Nani kakutieni damu mpya? Mlikuwa watulivu nyinyi …
We… wewe… (Mlinzi anamfikia na kumkamata mkono
mwari)
Mwari I: Nyeupe ni nyeupe na nyeusi ni nyeusi … na nyekundu ni
nyekundu, nyekundu haiwezi kuwa manjano …
Mlinzi I: Sharrab! Unajuaje wewe? Nyeupe ni nyeusi na nyeusi ni
nyeupe na nyekundu kila siku ni manjano …
134 Kitabu cha Mwanafunzi
Kidato cha Tano
23/06/2024 17:54
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 134 23/06/2024 17:54
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 134