Page 150 - Fasihi_Kisw_F5
P. 150
Fasihi ya Kiswahili kwa Shule za Sekondari
Mwenyekiti wa Jopo: Bi. Nagona, jopo limekusikiliza na kukagua vyeti
vyako. Tunakuruhusu uende. Nasi tunaendelea
kukamilisha mchakato huu. Tutakujulisha
matokeo yoyote yatakayoamuliwa kwa kutumia
FOR ONLINE READING ONLY
mawasiliano uliyoyaweka katika barua ya maombi
pamoja na taarifa za wasifu kazi wako.
Nagona: Asanteni sana, ninasubiri kwa hamu matokeo
hayo. Je, ni lini yanatarajiwa kuwa tayari?
Mwenyekiti wa Jopo: Ndani ya juma moja kuanzia leo utapata majibu.
Nagona: Asanteni, na kwa kwaherini.
Maswali
(i) Kwa nini unafikiri utambulisho ni muhimu katika usaili?
(ii) Je, unafikiri hoja za msailiwa zilikuwa na mantiki na ushawishi? Kwa
nini?
(iii) Ni maeneo yapi msailiwa ametumia maarifa ya kifasihi kujenga hoja
zake?
(iv) Ungekuwa Nagona, ungejibuje swali kutoka kwa Mjumbe wa 1,
Mjumbe wa 3 na Mjumbe wa 4?
(b) Tumia maarifa ya kifasihi kuwasilisha hoja zenye mantiki na ushawishi
wakati wa kuigiza kama msailiwa wa nafasi ya kazi.
(c) Tumia maarifa ya kifasihi kuwasilisha hoja zenye mantiki na ushawishi
wakati wa kuigiza kama mgombea wa nafasi ya uongozi katika uchaguzi
wa shuleni kwenu.
Shughuli ya 5.13
Chagua mada mojawapo kati ya zifuatazo, kisha andaa hoja unazoweza kuwasilisha
katika malumbano ya hoja kwa kutumia maarifa ya kifasihi kuwasilisha hoja
zenye mantiki na ushawishi.
(i) Athari za utandawazi kwa vijana
(ii) Mchango wa fasihi katika utunzaji wa mazingira
Kitabu cha Mwanafunzi 139
Kidato cha Tano
23/06/2024 17:54
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 139 23/06/2024 17:54
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 139