Page 154 - Fasihi_Kisw_F5
P. 154
Fasihi ya Kiswahili kwa Shule za Sekondari
hujumuisha matini iliyo katika umbo la utungo mmoja kama vile semi mbalimbali,
hadi matini zenye mchanganyiko wa mambo mengi. Mifano ya matini hizo ni
insha za kifasihi, ushairi, tamthiliya, hadithi fupi, na riwaya. Kazi changamani
ni zile zenye mchanganyiko wa mbinu nyingi za kisanaa. Pia, kazi hizi huwa
FOR ONLINE READING ONLY
na idadi kubwa ya vipengele kama vile vya wahusika, visa, mikasa, migogoro,
mandhari na dhamira.
Kubuni ni mchakato wa kusawiri mawazo kwa kutumia mbinu za kisanaa.
Mchakato huu huweza kufanyika katika nyuga mbalimbali, ambapo huanzia
akilini mwa mtu kisha hudhihirika kupitia maumbo mbalimbali. Katika uga
wa fasihi, ubunifu hujitokeza kupitia maumbo kama vile shairi, insha, hadithi,
riwaya, tamthiliya na utenzi. Watunzi wa kazi za fasihi huwa na kipaji, lakini
wengine huwa watunzi bora kwa kujifunza. Kazi ya kubuni hutakiwa iwe na sifa
kama vile: fikra za kisanaa kuhusu jambo au tukio; lengo au ujumbe maalumu;
upya wa namna fulani; umuhimu kwa jamii, na izingatie maslahi na maadili ya
jamii.
Uandishi wa kazi za fasihi ni mchakato wa kiubunifu. Katika kuandika kazi za
fasihi, msanii au mwandishi huanza kwa kujiuliza maswali kadha wa kadha.
Baadhi ya maswali hayo ni: Anaandika kuhusu nini? Anamwandikia nani?
Anaandika kwa kutumia mandhari ipi? Lengo lake ni nini? Na, anaandika kwa
namna gani? Kwa kuwa mwandishi huandika kazi yake ili isomwe na watu
wengine, hana budi kuzingatia mahitaji na mitazamo ya wasomaji wake ili aweze
kuwapeleka anakotaka huku wakiendelea kufurahia kusoma kazi husika.
Waandishi wa kazi za fasihi huandika kazi zao kwa malengo tofauti. Miongoni
mwa malengo hayo ni kusawiri uhalisi wa kijamii ili kuurekebisha au hata
kuubadili ikibidi. Hii ina maana kuwa mwandishi sharti aibuke na vitu vipya
ambavyo vitawavutia wasomaji katika kuwahabarisha yale yanayotokea katika
jamii yao. Vilevile, waandishi wa kazi za fasihi huandika kwa lengo la kuelezea
hisia zao ambazo wanaamini kuwa zitawavutia wasomaji wao ili wayaone
maisha kama wanavyoyaona wao. Pia, waandishi wanaandika ili kuwaburudisha
wasomaji wao. Hii inatokana na ukweli kuwa katika mchakato wa usomaji,
msomaji hupata maarifa na burudani. Halikadhalika, waandishi huandika ili
kuwashawishi wasomaji wao wakubali ukweli na namna ya kufasili mambo
mbalimbali kama wanavyofanya wao. Mbali na hayo, waandishi huandika kwa
lengo la kujipatia fedha kutokana na mauzo ya kazi hizo. Baadhi ya waandishi
huandika ili watambuliwe na jamii zao.
Kitabu cha Mwanafunzi 143
Kidato cha Tano
23/06/2024 17:54
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 143 23/06/2024 17:54
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 143