Page 149 - Fasihi_Kisw_F5
P. 149
Fasihi ya Kiswahili kwa Shule za Sekondari
mimi kama dhahabu iliyo katikati ya mchanga.
Pili, ni uzoefu nilioupata katika kufundisha somo
la Kiswahili katika shule za sekondari wakati wa
mafunzo kwa vitendo na wakati wa ufundishaji
FOR ONLINE READING ONLY
wa kujitolea baada ya kuhitimu masomo yangu ya
elimu ya juu.
Mjumbe 2: Una ahadi au matumaini gani ya kipekee
unayotupatia ikiwa tutakuajiri?
Nagona: Ninaahidi kuigeuza taasisi hii kuwa kijiji imara
cha wataalamu wa Kiswahili.
Mjumbe 3: Kufanya kazi katika taasisi kama hii kuna
changamoto nyingi. Je, unazifahamu changamoto
hizo? Na umejiandaaje kuzikabili?
Nagona: Ninatambua kuwa taasisi kama hii ambayo
hujumuisha watu wengi lazima itakuwa na
changamoto. Mfano wa changamoto hizo ni kuwapo
kwa akili na mitazamo tofauti ya kuyakabili masuala
kadha wa kadha, wingi wa mambo yanayotokea,
na masuala mengine yanayoendana na tabia za
watu. Hata hivyo, nimewahi kusoma riwaya
moja iitwayo Kusadikika ambayo mhusika wake
mkuu, Karama, alinifundisha kuwa mapambano
ya maisha yanahitaji vitu vikubwa vitatu ambavyo
ni ubongo wenye utulivu, ulimi wenye staha, na
moyo wenye ujasiri na saburi. Ninalihakikishia
jopo hili kuwa nitatumia zana hizo tatu kukabiliana
na changamoto zitakazotokea hapa. Ijapokuwa
natambua kuwa si kazi rahisi, bali penye nia pana
njia, hivyo ninatia nia ya kufanikiwa kuzikabili.
Mjumbe wa 4: Bi. Nagona una matarajio gani kuhusu kiasi cha
mshahara kama ukipata kazi hii?
Nagona: Ninashukuru sana kwa swali hili. Matarajio yangu
ni kulipwa kufuatana na viwango vya mishahara
vinavyoendana na ujuzi na elimu yangu.
138 Kitabu cha Mwanafunzi
Kidato cha Tano
23/06/2024 17:54
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 138 23/06/2024 17:54
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 138