Page 151 - Fasihi_Kisw_F5
P. 151
Fasihi ya Kiswahili kwa Shule za Sekondari
(iii) Nafasi ya lugha ya Kiswahili katika kukuza uchumi wa taifa
(iv) Dhima ya lugha ya Kiswahili katika kuleta umoja wa Afrika ya Mashariki.
Kutumia maarifa ya kifasihi kuwasilisha hoja zenye mantiki na ushawishi
katika malumbano ya hoja
FOR ONLINE READING ONLY
Malumbano ya hoja ni jukwaa muhimu katika kuwasilisha masuala mbalimbali.
Vilevile, ni nafasi nzuri ya kukuza maarifa ya kujenga hoja zenye mantiki
na ushawishi. Katika ulimwengu wa kidijiti, malumbano ya hoja yanaweza
kufanyika kwa kutumia vyombo vya habari kama vile runinga, redio na majukwaa
ya mtandaoni. Wahusika hupeana mada kwa ajili ya kufanya maandalizi (yaani
kuandaa taarifa za msingi, ushahidi na kupangilia mawazo kimantiki), kisha
hukutana kwa ajili ya uwasilishaji. Kwa kawaida, hoja huwekwa mezani kisha
kila mmoja hutoa mawazo yake kulingana na uelewa wa hoja hiyo. Ni muhimu
kupeana nafasi wakati wa uchangiaji wa mawazo ili kuruhusu maelewano na
kuheshimu mawazo ya mwingine katika mjadala. Vilevile, malumbano ya hoja
huongeza maarifa ya usikivu.
Shughuli ya 5.14
Andaa hoja zenye mantiki na ushawishi unazoweza kuziwasilisha katika
malumbano ya hoja kuhusiana na mada yoyote kwa kutumia maarifa ya kifasihi.
Tamrini
1. Kwa kutumia mifano, fafanua mbinu zinazotumika kujenga ujumi.
2. “Kujenga hoja kimantiki hakuna tija yoyote” Jadili hoja hii kwa mifano
thabiti.
3. Eleza namna utakavyojenga hoja zenye mantiki na ushawishi kwa
kutumia misingi ya kifasihi.
4. Fafanua namna misingi ya kifasihi inavyoweza kutumika kutathimini
matendo ya wahusika katika kazi ya fasihi.
5. Kwa kutumia mada ya ‘athari za dawa za kulevya kwa watoto wa
mtaani’, andaa hoja zenye mantiki na ushawishi.
6. Tumia misingi ya kujenga hoja zenye mantiki kutathmini maudhui ya
simulizi yoyote.
140 Kitabu cha Mwanafunzi
Kidato cha Tano
23/06/2024 17:54
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 140 23/06/2024 17:54
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 140