Page 146 - Fasihi_Kisw_F5
P. 146
Fasihi ya Kiswahili kwa Shule za Sekondari
Mlinzi II: (Anamkamata mwari 2) Nimekukamata sasa … kwa
nini ukaniendesha mbio? Kwa nini unanitimua? Tazama,
unaona n’navyohema hivi? Pumzi juujuu, kwa nini?
Mmekuwa kama mang’ombe yaliyovunja zizi kwa njaa
na kiu ilhali mnashiba? Kwa nini hamtaki kushiba utulivu
FOR ONLINE READING ONLY
wa miaka mingi uliopo Giningi? Kwa nini mnaona kiu
kwenye maji safi? Nyinyi waharibifu …
Mwari II: Mchana ni mchana na usiku ni usiku; na ikiwa kumekucha
basi kumekucha; asemaye bado ni usiku wa manane ni
mwongo …
Mlinzi III: Nani mwongo hapa enh? (Anamwelekeza nalo rungu,
lakini mwari anarudi nyuma)
Mwari III: Haijapata kutokea fujo hapa Giningi. (Huku akimfukuza
… Mwari III anapiga kelele)
Mlinzi IV: Mmekula … mmeshiba; mmelishwa sumu nini nyinyi?
Sumu gani? Na nani? Ah, mnataka kutwambia nini sasa?
Mnataka kutwambia kwamba kuanzia leo jua halitatoka
Magharibi na kuzama Mashariki? Mnataka kutwambia
kwamba mchana kuna jua na usiku kuna kiza? Nani kasema
hayo? Mmejigeuza watume wapya nyinyi mnakuja kuleta
wahyi mpya hapa Giningi? Ah, wako wapi wafalme wetu
wa Giningi? Nyinyi …
Mwari IV: Ndiyo … tunasema ndiyo, sote kwa umoja wetu, sasa
tunaliona jua halitoki Magharibi: jua linatoka Mashariki
na kuchwea Magharibi; hiyo ndiyo kanuni ya mwenendo
wa jua enzi na azali! Ulimwenguni kote… na … na …
(Anahema) usiku usio mbalamwezi na nyota ni kiza …
kiza kitupu … na mchana usiyo mawingu ni mwangafu
kwa jua linalodanda …
Mlinzi V: Ngoja utaona … (Kwa mwari V)
Walinzi na wari wengine wanaingia na kutoka na sauti za mabishano
zinazopandana na kuingiliana huku wakifukuzana na zogo na ghasia …
Kivuli kinaishi (Mohamed, 2009:103-104)
Kitabu cha Mwanafunzi 135
Kidato cha Tano
23/06/2024 17:54
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 135 23/06/2024 17:54
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 135