Page 156 - Fasihi_Kisw_F5
P. 156
Fasihi ya Kiswahili kwa Shule za Sekondari
Muktadha wa kijiografia hujumuisha vipengele kama vile: sura ya nchi, uoto,
bahari, maziwa, mito, na hali ya hewa. Vipengele hivi vina nguvu ya kushawishi
kuandika kazi ya fasihi. Aghalabu, kazi zinazotokana na msukumo wa kijiografia
husawiri masuala ya mazingira. Mwandishi anaweza kutunga hadithi, mashairi,
riwaya au tamthiliya zinazojadili masuala ya viumbe hai na mazingira ya asili
FOR ONLINE READING ONLY
kulingana na uzoefu wake.
Mbali na miktadha hiyo, uandishi wa kazi za kifasihi, kwa kiasi kikubwa,
huchochewa na maisha ya mwandishi na uzoefu wake binafsi. Mambo haya
huibua hisia, matukio muhimu maishani, na changamoto anazokutana nazo
mwandishi. Hayo yote humchochea mwandishi kuandika utungo wa kiubunifu
ili kuyawasilisha kwa wengine. Hata hivyo, licha ya kuwa kila mwandishi ana
vyanzo vyake vya kipekee vinavyomchagiza kuandika kazi za fasihi ni muhimu
kujifunza kutoka kwa wengine, na wakati huohuo kudumisha msukumo wa ndani
wa kuandika ili kuendeleza uwezo wake wa kiubunifu katika uandishi wa kazi
za kifasihi.
Zoezi la 6.1
1. Eleza maana ya kutunga kazi changamani za kifasihi.
2. Jadili dhana ya muktadha katika utunzi wa kazi za kifasihi.
3. “Fasihi ni zao la kisiasa”. Jadili kauli hii kwa mifano thabiti.
4. Fafanua namna masuala ya kijamii yanavyochagiza utunzi wa kazi za
kifasihi.
5. Jadili namna utunzi wa kazi za kifasihi unavyoweza kuchochewa na
muktadha wa kiutamaduni.
Shughuli 6.2
Tumia maktaba na vyanzo vya mtandaoni, eleza fursa mbalimbali zinazotokana
na kazi za kifasihi za Kiswahili.
Fursa zinazotokana na kazi za kifasihi
Ubunaji wa kazi za kifasihi unatoa fursa nyingi ambazo humwezesha msanii
binafsi, kikundi na mashirika kukuza kipato kutokana na mchakato wa kuhariri,
kuchapisha, kusambaza, na kuuza kazi za kifasihi. Vilevile, uandishi wa kazi za
Kitabu cha Mwanafunzi 145
Kidato cha Tano
23/06/2024 17:54
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 145 23/06/2024 17:54
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 145