Page 159 - Fasihi_Kisw_F5
P. 159
Fasihi ya Kiswahili kwa Shule za Sekondari
Mchango wa TEHAMA katika kukuza fursa za utunzaji, usambazaji,
usomaji na uuzaji wa kazi za fasihi
Matumizi ya TEHAMA yamechangia sana katika kutambua fursa mbalimbali
zinazotokana na kazi za fasihi. Ufuatao ni mchango wa TEHAMA katika
FOR ONLINE READING ONLY
kutambua fursa hizo:
Mosi, TEHAMA ina mchango mkubwa katika kuchambua kazi za fasihi. Hii
inatokana na matumizi ya programu mbalimbali kama vile akili unde ambayo
hutumika katika kuchambua kazi za fasihi simulizi na andishi.
Pili, imewezesha uhifadhi na usambazaji wa kazi mbalimbali za kifasihi kwa
urahisi na haraka kupitia mitandao ya kijamii. Kutokana na hilo, hadhira
imekuwa ikitumia mitandao hiyo kusoma kazi hizo na kupata maarifa mbalimbali
yanayohusiana na kazi za fasihi.
Tatu, imesaidia kukuza hali za kiuchumi za watunzi kutokana na baadhi ya kazi
hizo kuwekwa mitandaoni na kuwataka wasomaji kuzilipia kabla ya kuzipakua
ili kuzisoma au kuzisikiliza.
Nne, imechangia kukuza usomaji wa kazi za kifasihi kupitia vyanzo mbalimbali
vya mtandaoni. Wasomaji hufungua programu mbalimbali ambazo huzisoma
wakati wowote na mahali popote na kujipatia maarifa kutoka katika kazi za fasihi
ya Kiswahili.
Tano, TEHAMA imerahisisha mawasiliano kwa sababu imewaunganisha
waandishi kwa kutumia majukwaa mbalimbali ya mitandao katika utendaji wao.
Majukwaa hayo ni kama vile, makundi ya WhatsApp na majukwaa mbalimbali
ya majadiliano. Majukwaa haya yamewezesha waandishi hao kushirikiana katika
kazi za uandishi na usambazaji wa kazi zao kwa urahisi.
Kwa ujumla, TEHAMA ina mchango mkubwa katika kuleta fursa mbalimbali
kwenye fasihi ya Kiswahili kwa kutoa njia za utunzaji, usambazaji, usomaji na
uingizaji wa kipato kwa watumiaji wa kazi za fasihi andishi.
Shughuli ya 6.4
Eleza jinsi TEHAMA inavyoweza kutoa fursa za kubidhaisha kazi ya kifasihi.
148 Kitabu cha Mwanafunzi
Kidato cha Tano
23/06/2024 17:54
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 148
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 148 23/06/2024 17:54