Page 158 - Fasihi_Kisw_F5
P. 158
Fasihi ya Kiswahili kwa Shule za Sekondari
na kuboresha stadi za uandishi. Vilevile, mhariri atakuwa na nafasi ya kushirikiana
na wahariri wengine katika kuboresha kazi mbalimbali.
Aidha, kazi za fasihi hutoa fursa ya kukuza na kuendeleza sanaa. Hii ni kutokana
na kuwepo kwa watu wenye vipaji na hata kujifunza kutoka kwa wengine kwa
FOR ONLINE READING ONLY
sababu ya kuangalia tamthiliya mbalimbali za ndani na nje ya nchi. Fursa hii
huwawezesha watu kuingia katika ulimwengu wa sanaa na kujipatia kipato.
Fursa nyingine ya kisanaa ni kuwa mchoraji katika kazi mbalimbali za kifasihi,
na vitabu vya watoto.
Fursa nyingine itokanayo na uandishi wa kazi za fasihi ya Kiswahili ni kuwa
mwalimu wa kuifundisha fasihi hiyo. Mwalimu humwezesha mwanafunzi
kujenga misingi ya fasihi ya Kiswahili na kuwahamasisha wanafunzi kupenda
kujisomea kazi mbalimbali za fasihi. Kadhalika, kazi za fasihi hutoa fursa ya
kuwa mwalimu wa kufundisha masuala ya uandishi wa kazi bunifu. Kazi hizo
za kibunifu zinaweza kuwa za hadithi/hadithi za watoto, riwaya, tamthiliya,
mashairi, na insha za kifasihi.
Kazi za fasihi humwezesha mtu kupata fursa ya kutafsiri vitabu vya fasihi. Tafsiri
hizi huweza kuwa za vitabu vilivyoandikwa kwa lugha za Kiafrika na lugha za
kigeni kwenda lugha ya Kiswahili na kinyume chake. Tafsiri hizo sharti zifanywe
na mtu ambaye ana ujuzi wa kazi za fasihi ili kufumbata vionjo vya kifasihi
katika lugha lengwa. Mfano wa vitabu vilivyotafsiriwa ni pamoja na tamthiliya za
Mabepari wa Venisi, Juliasi Kaizari, Mfalme Edipode na Nitaolewa Nikipenda;
na riwaya ya Barua Ndefu Kama Hii. Vitabu vilivyotafsiriwa huingia kwenye
ushindani wa kibiashara, hivyo huingiza kipato kwa mtafsiri.
Utunzi wa kazi za kifasihi humwezesha mtunzi kuwa mtafiti wa lugha na fasihi
ya Kiswahili. Kupitia utafiti mtu hujijengea ujuzi wa mitindo mbalimbali ya
uandishi wa kazi za kifasihi.
Kimsingi, kazi za fasihi ya Kiswahili hutoa fursa nyingi kwa jamii. Fursa hizo ni
kama za uaimbaji, uchoraji, uhariri, ualimu/uhadhiri, utafiti na uigizaji. Kazi zote
hutoa fursa za kujipatia kipato na kukuza uchumi binafsi na wa nchi.
Shughuli ya 6.3
Kwa kutumia majukwaa ya kidijiti kama vile Instagram, WhatsApp na Youtube
eleza mchango wa TEHAMA katika kuongeza fursa za kutangaza na kuuza kazi
za fasihi.
Kitabu cha Mwanafunzi 147
Kidato cha Tano
23/06/2024 17:54
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 147 23/06/2024 17:54
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 147