Page 161 - Fasihi_Kisw_F5
P. 161
Fasihi ya Kiswahili kwa Shule za Sekondari
kuandikia. Vilevile, mtunzi anapaswa kusoma kazi za utanzu husika, kuteua
hadhira, kuandaa vifaa atakavyohitaji, na kuandaa ratiba ya kazi. Kisha, anatakiwa
kuandika dondoo muhimu za kazi. Ufuatao ni ufafanuzi wa vipengele hivi
(b) Kubuni wazo au mada
FOR ONLINE READING ONLY
Uandishi wa kazi ya fasihi hujengwa katika wazo kuu ambalo ndilo huchanuza
mawazo madogomadogo ili kufikisha ujumbe kwa hadhira husika. Mtunzi wa kazi
ya fasihi anapaswa kubuni wazo au mada itakayowavutia wasomaji na kuwapa
hamasa ya kusoma kazi yake. Mada au wazo hilo linaweza kuwa la kufikirika, la
kihistoria au mada inayohusu masuala muhimu ya kijamii. Mwandishi anaweza
kupata wazo kutokana na uzoefu wake au mambo aliyoyapitia katika maisha
na miktadha mingine. Vilevile, anaweza kufanya utafiti ili kuelewa masuala
yanayogusa jamii yake, ambayo yatamsaidia kupata wazo la kuandikia. Mambo
yanayoigusa jamii yanaweza kuwa ya kijamii, kisiasa, kiuchumi na masuala
mtambuka. Ni vizuri mwandishi abuni mada anayoipenda na atakayoimudu
kuiandikia kazi yake.
(c) Kufanya uchunguzi
Baada ya kupata wazo au mada, mtunzi anaweza kukusanya taarifa anuai kuhusu
wazo alilolipata. Anaweza kusoma vitabu, makala, au hata kufanya utafiti kuhusu
wazo hilo. Lengo ni kupata maarifa ya kutosha na taarifa sahihi kuhusu wazo/
mada. Vilevile, uchunguzi humwezesha mtunzi kuelewa mazingira ya jamii,
historia, utamaduni, na masuala mengine yanayohusiana na wazo au mada
iliyochaguliwa.
(d) Kuamua kuhusu utanzu wa kuandika
Kila utanzu huwa na mtindo wake wa kiuandishi. Kwa hiyo, mtunzi anapaswa
kuamua kuhusu utanzu atakaoutumia katika kuwasilisha wazo au mada
aliyoibuni. Utanzu huo unaweza kuwa wa ushairi, tamthiliya, hadithi au riwaya.
Hii itamsaidia kufikisha ujumbe wake kwa kuzingatia muundo na mtindo wa
kiuandishi wa utanzu husika. Kwa mfano, ikiwa ni mashairi, mtunzi atapaswa
kuzingatia kaida mbalimbali za ushairi kama vile: muundo, mtindo, lugha ya
kishairi na mambo mengine yanayohusu ushairi. Ni vyema mwandishi akaandikia
utanzu anaoumudu.
(e) Kusoma kazi za utanzu husika
Usomaji wa kazi husika za fasihi humpa mwandishi fursa ya kujifunza kutoka
kwa waandishi wengine, ili kupata maarifa na kuimarisha stadi ya kuandika. Pia,
humsaidia mtunzi kuwa na uelewa mzuri wa vipengele vya uandishi kama vile
150 Kitabu cha Mwanafunzi
Kidato cha Tano
23/06/2024 17:54
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 150 23/06/2024 17:54
FASIHI YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI KIDATO CHA TANO.indd 150