Page 6 - Historiayatznamaadili
P. 6
Utangulizi
Kitabu cha Historia ya Tanzania na Maadili kimeandikwa
FOR ONLINE READING ONLY
mahususi kwa ajili ya mwanafunzi wa Darasa la Nne, Tanzania
Bara. Kitabu hiki kimeandaliwa kulingana na muhtasari wa somo
la Historia ya Tanzania na Maadili uliotolewa na Wizara ya Elimu,
Sayansi na Teknolojia mwaka 2023.
Kitabu hiki kina sura nane, nazo ni: Wajibu na haki za mtoto
katika jamii na Taifa, Maendeleo ya jamii kabla ya ukoloni,
Sayansi na teknolojia za asili kabla ya ukoloni, Shughuli za
uchumi kabla ya ukoloni, Ushirikiano na uhusiano wa kijamii
na kiuchumi, Mamlaka za jadi kabla ya ukoloni, Mamlaka za
jadi katika ukuzaji na utunzaji wa maadili, na Alama za Taifa
na utambullisho wa Taifa. Maudhui ya kitabu cha Historia ya
Tanzania na Maadili Darasa la Nne yamejikita zaidi katika historia
ya Tanzania na maadili na watu wake kabla ya ukoloni. Kwa
kujifunza maudhui ya kitabu hiki, mwanafunzi atamudu historia
ya Tanzania na maadili yake kabla ya ukoloni. Aidha, maudhui
haya yatamwezesha kumudu maarifa, stadi na mwelekeo wa
kuwa mzalendo, kujenga maadili, kukuza utaifa na kulinda
rasilimali anuwai za Taifa zilizojengwa kwa vipindi tofauti nchini.
Hivyo, kumwezesha kuishi katika misingi ya utu, uadilifu, umoja,
upendo, amani na kuthamini rasilimali za Taifa na watu wake
pasipokujali rangi, dini, jinsi zao, wala mahali wanapotoka.
Maudhui ya sura hizi yamewasilishwa kwa njia ya matini, kazi za
vitendo, picha zenye mvuto na mazoezi. Kwa hiyo, mwanafunzi
anapaswa kufanya mazoezi na kazi zote zilizopo kwenye kitabu
hiki pamoja na kazi nyingine atakazopewa na mwalimu ili kufikia
lengo la somo la Historia ya Tanzania na Maadili kwa Darasa
la Nne.
v
06/11/2024 11:29:24
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 5
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 5 06/11/2024 11:29:24