Page 8 - Historiayatznamaadili
P. 8
Sura ya Wajibu na haki za mtoto
Kwanza katika jamii na Taifa
FOR ONLINE READING ONLY
Utangulizi
Wajibu na haki za mtoto ni muhimu kwa maendeleo ya mtoto katika jamii
na Taifa. Ulipokuwa Darasa la Tatu, ulijifunza kuhusu wajibu na haki za
mtoto shuleni na nyumbani. Katika sura hii, utajifunza kuhusu wajibu na
haki za mtoto katika jamii na Taifa. Umahiri utakaoupata utakuwezesha
kutambua wajibu na haki za mtoto katika jamii na Taifa. Hivyo, kukuwezesha
kutekeleza wajibu wako ili kurahisisha kupata haki zako katika jamii na
Taifa kwa ujumla.
Fikiri
Wajibu na haki za mtoto katika jamii na Taifa.
Dhana ya wajibu na haki za mtoto
Kazi ya kufanya namba 1
Soma matini kutoka vyanzo mbalimbali, ikiwamo
maktaba mtandao kuhusu wajibu na haki za mtoto
katika jamii na Taifa.
Wajibu ni mambo ya lazima ambayo mtu hupaswa kuyatenda
ili kukabili mazingira yanayomzunguka. Wajibu huambatana
na sheria za jamii na Taifa ambazo ni lazima kuzitekeleza na
kuzitimiza. Hii ina maana usipotimiza wajibu, utaonekana kuwa
mtu wa tofauti. Ibara ya 25-28 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania inaeleza kuhusu wajibu wa Watanzania wote na
1
06/11/2024 11:29:25
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 1 06/11/2024 11:29:25
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 1