Page 12 - Historiayatznamaadili
P. 12
Kazi ya kufanya namba 3
Jadili na andika matendo yanayoashiria mtoto
kuheshimiwa, kutambuliwa na kuthaminiwa utu wake
FOR ONLINE READING ONLY
katika jamii.
Kulindwa na kupata haki sawa
Kila mtoto ana haki ya kulindwa dhidi ya mateso, vitisho na
kupewa adhabu zinazomdhalilisha. Kimsingi, haki hii inahusu
ulinzi wa mtoto dhidi ya ukatili, unyanyasaji, uonevu na udhalilishaji
wa aina yoyote katika jamii yake na Taifa. Vyombo vya ulinzi
kuanzia ngazi za Mtaa/Kijiji, Kata hadi Taifa vimewekwa kwa ajili
ya ulinzi na usalama wa mtoto. Aidha, endapo mtoto atafanyiwa
vitendo vya ukatili, unyanyasaji, uonevu na udhalilishaji, ana
wajibu wa kutoa taarifa katika vyombo vya usalama ili kupata
msaada.
Kazi ya kufanya namba 4
Chunguza na andika zilipo ofisi za Mtaa/Kijiji, Kata
na Taifa maeneo yanayokuzunguka ambapo mtoto
anaweza kutoa taarifa iwapo haki zake zitakiukwa.
Kusikilizwa kwa ukamilifu
Mtoto ana haki ya kushiriki na kujadili masuala yanayomhusu
katika mikutano na vikao katika jamii inayomzunguka. Hivyo, ana
haki ya kutoa mawazo yake bila kuathiri sheria za nchi katika
jamii na Taifa. Haki hii humpa mtoto nafasi ya kushiriki katika
kutoa uamuzi wa masuala yanayohusu ustawi wake. Mtoto ni
raia kama walivyo raia wengine katika serikali ya Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania.
5
06/11/2024 11:29:28
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 5
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 5 06/11/2024 11:29:28