Page 17 - Historiayatznamaadili
P. 17
pamoja na wananchi. Pia, inaelezea wajibu wa kuheshimu mali
ya mtu mwingine. Watu wote wanatakiwa kupiga vita uharibifu na
ubadhirifu wa mali za umma na za jamii na kuendesha uchumi
wa Taifa kwa umakini kwa ajili ya kizazi cha sasa na kijacho.
Hivyo, mtoto ana wajibu wa kutunza na kulinda maliasili za
FOR ONLINE READING ONLY
Taifa, mali za umma na za jamii na kutokushiriki vitendo vya
uharibifu wake. Pia, mtoto ana wajibu wa kushiriki katika kutoa
elimu na kuandaa kampeni za kutunza mali za umma katika
jamii. Mfano, mtoto anaweza kufanya kampeni kwa kushiriki
shughuli za kutunza mazingira katika jamii. Kielelezo namba 5,
kinaonesha watoto wakishiriki kazi za kupanda miti.
Kazi ya kufanya namba 10
Andaa klabu ya utunzaji na ulinzi wa mali zilizopo
katika jamii kwa kuonesha mikakati na utekelezaji
wake.
Kielelezo namba 5: Watoto wakishiriki kupanda miti
10
06/11/2024 11:29:31
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 10 06/11/2024 11:29:31
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 10