Page 18 - Historiayatznamaadili
P. 18
Kuonesha heshima na utii katika jamii
Mtoto ana wajibu wa kuheshimu watu waliomzidi umri, pamoja
na watoto wenzake bila ya kujali rangi, hali ya maisha au jinsi.
Heshima inaweza kuoneshwa kwa kusalimia watu wengine,
FOR ONLINE READING ONLY
kukubali kutumwa na kufanya kazi bila kuonesha kiburi. Pia,
mtoto anaweza kuonesha heshima kwa kuwasaidia wazee,
watu wenye mahitaji maalumu na watu wengine katika jamii
yake na Taifa kwa ujumla. Aidha, mtoto kuonesha unyenyekevu
na kukubali kuelekezwa katika mambo halali na ya msingi ni
sehemu ya kuonesha heshima na utii katika jamii. Wajibu huu ni
muhimu kwa mtoto ili kukubalika katika jamii. Licha ya kuonesha
heshima kwa watu wengine, mtoto ana wajibu wa kujiheshimu.
Kazi ya kufanya namba 11
Jadili na orodhesha matendo yanayoonesha
kujiheshimu na ya kutojiheshimu katika jamii
inayokuzunguka.
Matendo ya kujiheshimu kwa mtoto ni yale yanayokubalika na
jamii yake. Matendo ya kutojiheshimu ni yale yasiyokubalika
na jamii yake. Mtoto hapaswi kuiga na kutenda matendo yaliyo
kinyume na maadili ya jamii na Taifa lake. Pia, mtoto ana wajibu
wa kukubali na kufuata kanuni na sheria ambazo jamii imejiwekea
ili kuishi salama katika jamii yake.
Zoezi namba 2
1. Eleza umuhimu wa mtoto kujiheshimu katika jamii yake.
2. Je, kuna umuhimu gani wa mtoto kuwaheshimu watu
wengine katika jamii?
11
06/11/2024 11:29:31
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 11
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 11 06/11/2024 11:29:31