Page 19 - Historiayatznamaadili
P. 19
Kuzingatia maadili ya jamii
Ni wajibu wa mtoto kuzingatia maadili ya jamii na Taifa. Maadili
hayo ni pamoja na kuonesha uaminifu na uadilifu katika uhusiano
wake na watu wengine. Pia, ana wajibu wa kutojihusisha na
FOR ONLINE READING ONLY
vitendo vya rushwa na uhalifu mwingine kama vile matumizi
ya dawa za kulevya. Kwa kufanya hivyo, mtoto anaendeleza
maadili katika jamii yake na Taifa.
Kazi ya kufanya namba 12
Waulize wazazi au walezi kuhusu maadili ya jamii
inayokuzunguka na andika wajibu wako katika
kuyatekeleza.
Kushiriki katika shughuli za jamii na Taifa lake
Ni wajibu wa mtoto kushiriki katika shughuli za jamii na Taifa
lake. Mtoto anaweza kushiriki katika shughuli za jamii. Kwa
mfano, shughuli za mazishi, ibada, harusi, sherehe za kitaifa,
na shughuli zingine za maendeleo kulingana na umri wake. Pia,
mtoto anaweza kushiriki katika kazi mbalimbali katika jamii na
Taifa. Vilevile, anaweza kushiriki katika vikao vya maendeleo ya
jamii yake. Ushiriki huu, humjenga mtoto kimaadili na huonesha
kuwajibika katika jamii na Taifa. Pia, ushiriki humjengea mtoto
tabia ya kujali, kuhudumia na kuwajibika kwa wengine. Kielelezo
namba 6, kinaonesha ushiriki wa watoto katika kikao cha
maendeleo ya jamii.
12
06/11/2024 11:29:31
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 12
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 12 06/11/2024 11:29:31