Page 24 - Historiayatznamaadili
P. 24
FOR ONLINE READING ONLY
Kielelezo namba 7: Watoto wakishiriki kupinga rushwa
Kazi ya kufanya namba 17
Orodhesha miradi ya maendeleo inayotekelezwa na
serikali, kisha:
1. Andika faida ya jamii kushiriki katika kuzuia vitendo
vya rushwa katika miradi hiyo.
2. Andika madhara ya vitendo vya rushwa katika miradi
hiyo.
Kushirikiana na watoto wengine katika jamii na Taifa
Watoto ndio tegemeo la jamii na Taifa. Hivyo, ni wajibu wa
mtoto kushirikiana na watoto wengine katika jamii na Taifa ili
kujenga misingi ya maendeleo ya jamii zao. Ushirikiano na
watoto wengine katika jamii na Taifa huwajengea uwezekano
wa kufanya kazi pamoja sasa na baadaye. Pia, hujenga umoja
wa watoto kitaifa. Hivyo, ni wajibu wa watoto, kushirikiana na
watoto wengine ili kujenga uhusiano na umoja kati yao kwa
maendeleo ya jamii na Taifa.
17
06/11/2024 11:29:34
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 17
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 17 06/11/2024 11:29:34