Page 22 - Historiayatznamaadili
P. 22
jamii moja na nyingine. Hivyo, ni wajibu wa mtoto kujifunza
mambo mema ya utamaduni wa jamii yake na Taifa lake, ili
kuishi kulingana na mahitaji ya jamii yake na Taifa lake.
Kazi ya kufanya namba 15
FOR ONLINE READING ONLY
Waulize wazazi au walezi kuhusu mila na desturi
za jamii yako, kisha andika wajibu wako katika
kuzitekeleza.
Kimsingi, mtoto ana wajibu wa kujifunza na kuendeleza
utamaduni wa jamii inayomzunguka. Hivyo, mtoto anapaswa
kujifunza utamaduni wa jamii yake kutoka kwa wazazi, walezi na
watu wengine katika jamii. Aidha, mtoto ana wajibu wa kujifunza
na kuheshimu mila na desturi zinazoendeleza amani, utulivu,
utu na heshima.
Kujilinda na kujijali
Mtoto anao wajibu wa kujilinda na kujijali. Kujilinda ni kujikinga
dhidi ya mazingira hatarishi kwa kuepuka kuwa katika maeneo
hatarishi. Mfano, kutokutembea usiku, kutokwenda katika
vilabu vya pombe au magenge ya wavuta bangi na dawa za
kulevya. Mtoto hapaswi kuangalia picha chafu kwenye mitandao
ya kijamii au kujihusisha katika urafiki wa kimapenzi akiwa na
umri mdogo. Mtoto anatakiwa kuwa katika maeneo salama na
kuepuka maeneo ya uficho na kujitenga na watoto wengine.
Pia, mtoto hapaswi kuiga vitendo viliyo kinyume na maadili ya
jamii na Taifa lake.
Kazi ya kufanya namba 16
Jadili namna mtoto anavyoweza kujilinda na
kujijali katika mazingira yake.
15
06/11/2024 11:29:34
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 15
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 15 06/11/2024 11:29:34