Page 25 - Historiayatznamaadili
P. 25
Kazi ya kufanya namba 18
Jadili namna mtoto anavyoweza kushirikiana na
watoto wengine katika jamii na Taifa.
FOR ONLINE READING ONLY
Wajibu huu wa mtoto, umeambatana na sheria, hivyo, mtu
anapokiuka wajibu anaweza kuchukuliwa hatua za kisheria.
Kazi ya kufanya namba 19
Jadili mambo uliyojifunza kuhusu wajibu wa mtoto
katika jamii na Taifa.
Umuhimu wa wajibu na haki za mtoto katika jamii na Taifa
Kazi ya kufanya namba 20
Jadili umuhimu wa haki na wajibu wa mtoto katika
jamii na Taifa.
Wajibu na haki za mtoto ni muhimu kwa mtoto binafsi, jamii na
Taifa. Haki na wajibu wa mtoto ni muhimu kwani husaidia kuleta
ulinzi, heshima na fursa kwa watoto katika jamii na Taifa. Pia,
mtoto anayetambua haki na wajibu wake, hutekeleza wajibu
wake, na hudai haki zake. Hivyo, kumwezesha kupata haki zake
katika jamii na Taifa. Aidha, jamii inayotambua haki na wajibu
wa mtoto inaweza kumsaidia mtoto kutimiza wajibu wake. Hivyo,
kupata haki zake. Kwa ujumla haki na wajibu humsaidia mtoto:
(a) Kujikinga dhidi ya ukatili, unyanyasaji na udhalilishaji
kwa mtoto; Mtoto anayetambua haki zake katika jamii na
Taifa ni rahisi kufahamu vitendo vilivyo kinyume na haki
zake. Hivyo, kuchukua hatua za kujilinda kwa kudai haki
zake. Pia, huweza kutoa taarifa katika vyombo na mamlaka
zinazohusika au mashirika yanayoshughulikia masuala
ya watoto. Vilevile, anaweza kuwasaidia watoto wenzake
18
06/11/2024 11:29:34
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 18
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 18 06/11/2024 11:29:34