Page 27 - Historiayatznamaadili
P. 27
Kimsingi, wajibu na haki za mtoto katika jamii huweka mazingira
ya mtoto kushiriki katika ujenzi wa jamii na Taifa bora, na hivyo,
kujipatia mahitaji yake. Pia, husaidia mtoto kupata ulinzi, na
kuwa salama katika jamii. Jamii inayozingatia haki za mtoto na
yenye watoto wanaotimiza wajibu wao, huwa ni mahali salama
FOR ONLINE READING ONLY
pa kuishi.
Zoezi la jumla
1. Andika neno NDIYO mbele ya sentensi ambayo ni kweli
na neno HAPANA mbele ya sentensi ambayo si kweli.
(i) Mtoto hana haki ya kusikilizwa kwa ukamilifu katika
jamii yake _________________
(ii) Haki za mtoto ni kinga dhidi ya ukatili, unyanyasaji na
udhalilishaji kwa mtoto _________________
(iii) Wajibu na haki za mtoto katika jamii ni muhimu katika
kuimarisha ustawi wa kijamii na Taifa _____________
(iv) Ni haki ya mtoto kuonesha heshima na utii katika
jamii ______________
(v) Ni wajibu wa mtoto kuheshimu viongozi wa
serikali_____________
2. Eleza kwa kifupi wajibu wa mtoto katika jamii.
3. Fafanua umuhimu wa mtoto kutimiza wajibu wake katika
jamii na Taifa.
4. Taja mahali pa kutoa taarifa iwapo haki zako na za watoto
wengine zitavunjwa.
5. Je, jamii ina nafasi gani katika kukuza na kulinda haki za
mtoto?
20
06/11/2024 11:29:35
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 20
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 20 06/11/2024 11:29:35