Page 31 - Historiayatznamaadili
P. 31
Kazi ya kufanya namba 3
Jadili mambo yanayoashiria maendeleo ya jamii.
FOR ONLINE READING ONLY
Maendeleo ya jamii hutafsiriwa kwa kuangalia uwezo wa
wanajamii wa kuyakabili mazingira yao. Pia, huangaliwa katika
uwezo wa jamii wa kujipatia mahitaji yake, kujitegemea na
kusimamia mipango ya maendeleo. Vilevile, huangaliwa katika
uwezo wa kutumia rasilimali zilizopo katika mazingira kama
vile rasilimali watu, vitu, fedha, ardhi, pamoja na sayansi na
teknolojia ya jamii katika kutatua changamoto zao. Maendeleo
hayapaswi kuangaliwa kwa kulinganisha jamii moja na nyingine
tu, kwani jamii hutofautiana katika rasilimali walizonazo.
Umuhimu wa maendeleo ya jamii
Maendeleo ya jamii ni muhimu kwa ustawi wa mtu binafsi,
jamii na Taifa. Mfano, maendeleo katika elimu husaidia kukuza
maarifa na ujuzi wa jamii katika utendaji wa kazi. Aidha, elimu
huongeza ufanisi katika shughuli za uchumi na maendeleo
ya jamii. Maendeleo katika afya huboresha afya ya jamii, kwa
maana ya kukinga na kuponya jamii na magonjwa. Maendeleo
katika afya huwezesha kuwa na jamii yenye afya njema na
inayoshiriki kikamilifu katika kuleta maendeleo ya jamii na Taifa.
Vivyo hivyo, maendeleo katika miundombinu kama vile barabara,
miradi ya maji na umeme huongeza fursa za kiuchumi. Pia,
makazi bora husaidia jamii kuwa na mahali salama pa kuishi na
huiwezesha jamii kufanya kazi za kujiletea maendeleo binafsi
na ya Taifa. Kimsingi, maendeleo ya jamii ni msingi wa ustawi
wa jamii inayohusika.
Maendeleo ya jamii kabla ya ukoloni
Kabla ya kuja kwa wakoloni, jamii za Kitanzania zilikuwa na
maendeleo kadhaa katika afya, elimu na makazi. Maendeleo
hayo yaliwezesha watu kupata huduma za afya, elimu na kuishi
katika makazi bora.
24
06/11/2024 11:29:36
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 24
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 24 06/11/2024 11:29:36