Page 34 - Historiayatznamaadili
P. 34
Mbinu za utoaji wa elimu
Kazi ya kufanya namba 7
Waulize wazazi au walezi kuhusu mbinu zilizotumika
FOR ONLINE READING ONLY
kutoa elimu katika jamii inayowazunguka kabla ya
ukoloni.
Mbinu ya vitendo ilitumika zaidi kufundishia. Wanajamii
walielekezwa jinsi ya kutenda wakati kazi zikifanyika. Kielelezo
namba 3, kinaonesha vijana wakifundishwa maarifa na stadi
katika shughuli za uvuvi.
Kielelezo namba 3: Vijana wakifundishwa kuvua samaki
Pia, vijana walifundishwa kwa kushirikiana na wazazi wakifanya
kazi pamoja. Hii ilisaidia kuwashirikisha vijana maarifa na stadi
za jamii. Kielelezo namba 4, kinaonesha binti akijifunza stadi za
ufinyanzi akishirikiana na mzazi.
27
06/11/2024 11:29:39
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 27
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 27 06/11/2024 11:29:39