Page 39 - Historiayatznamaadili
P. 39
Nyumba za msonge
Kazi ya kufanya namba 10
Soma matini kwenye mtandao na maktaba mtandao
FOR ONLINE READING ONLY
kuhusu nyumba za msonge.
Nyumba za msonge zina umbo la duara juu na chini. Nyumba
hizo hujengwa kwa nyasi chini au fito zilizokandikwa kwa udongo
na kuezekwa juu kwa nyasi. Mfano wa nyumba hizo ni zile za jamii
za Wachaga, Waha na Wahaya. Nyumba nyingine za msonge
zilijengwa kwa miti pekee au miti na tope, kisha kuezekwa
kwa miti na nyasi ngumu. Mfano wa nyumba hizo ni zile
za jamii za Wanyakyusa na Wangoni. Kielelezo namba 6,
7 na 8, vinaonesha mfano wa nyumba za msonge zilizojengwa
kwa nyasi chini na kuezekwa juu kwa nyasi.
Kielelezo namba 6: Nyumba ya msonge ya jamii ya Wachaga
32
06/11/2024 11:29:42
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 32
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 32 06/11/2024 11:29:42