Page 43 - Historiayatznamaadili
P. 43
Nyumba za tembe
Nyumba za tembe zilijengwa kwa kutumia miti iliyosukwa kwa
kamba na fito, kisha kukandikwa kwa udongo ili ziwe imara.
Nyumba hizi hushikiliwa na nguzo imara. Nyumba za tembe
FOR ONLINE READING ONLY
huezekwa nyasi na miti, kisha kukandikwa kwa udongo juu.
Nyumba hizi zilikuwa fupi na zenye umbo la mstatili. Nyumba za
tembe zilijengwa na jamii zilizoishi mkoa wa Dodoma, Singida
na Manyara. Dodoma zilijengwa na jamii za Wagogo, Singida
na jamii za Wanyaturu na Wanyiramba na Manyara na jamii za
Wairaqw. Kielelezo namba 12, 13 na 14, vinaonesha mfano wa
nyumba za tembe.
Kielelezo namba 12: Nyumba ya tembe iliyojengwa kwa miti chini na
kufunikwa kwa udongo juu
Kielelezo namba 13: Nyumba ya tembe ya jamii za Wagogo na
Wanyaturu iliyojengwa kwa udongo juu na chini
36
06/11/2024 11:29:46
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 36
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 36 06/11/2024 11:29:46