Page 48 - Historiayatznamaadili
P. 48
Msamiati
Elimu mfumo wa kurithisha maarifa na stadi kutoka kizazi
kimoja hadi kingine
FOR ONLINE READING ONLY
Fito miti midogo mirefu mfano wa fimbo zilizosukwa
kwa kamba kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za asili
Jando mafunzo ya nadharia na vitendo kwa wavulana
kuhusu maisha, mila na desturi za jamii
Misemo mafungu ya maneno yanayotumiwa kwa ajili ya
kutoa maadili kwa jamii
Ufinyanzi ufundi wa kutengeneza vyombo vya udongo
Ukoloni mfumo wa Taifa moja kuvuka mipaka yake na
kutawala Taifa lingine kiuchumi, kisiasa na
kiutamaduni
Unyago mafunzo ya nadharia na vitendo kwa wasichana
kuhusu maisha, mila na desturi za jamii
Vitendawili semi zinazotolewa kwa njia ya fumbo lenye pande
mbili, upande mmoja ukiuliza na mwingine ukijibu
Wakunga watu waliotumika kutoa huduma za uzazi na
kuzalisha watoto
41
06/11/2024 11:29:48
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 41
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 41 06/11/2024 11:29:48