Page 52 - Historiayatznamaadili
P. 52
FOR ONLINE READING ONLY
Kielelezo namba 2: Zana za Zama za Mawe za Kale
Zama za Mawe za Kati
Sayansi na teknolojia iliendelea kukua zaidi wakati wa Zama
za Mawe za Kati. Binadamu alitengeneza zana bora zaidi na
nyepesi zikilinganishwa na zile za Zama za Mawe za Kale. Zana
za Zama za Mawe za Kati, zilikuwa bora na imara zaidi kwa ajili
ya kufanyia kazi mahususi. Binadamu alibuni na kutengeneza
kwa ustadi zana nyingi na tofauti kwa matumizi. Mfano, binadamu
alitengeneza mishale, visu, mikuki na mashoka kwa kutumia
mawe. Kielelezo namba 3, kinaonesha baadhi ya mifano ya
zana za Zama za Mawe za Kati.
Kielelezo namba 3: Zana za Zama za Mawe za Kati
45
06/11/2024 11:29:51
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 45 06/11/2024 11:29:51
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 45