Page 55 - Historiayatznamaadili
P. 55
FOR ONLINE READING ONLY
Kielelezo namba 5: Zana za Zama za Mawe za Mwisho
Binadamu alianza kuwekea mipini baadhi ya zana za mawe
kama vile mashoka, mikuki na mishale. Mipini iliwezesha zana
kuwa imara zaidi katika utumiaji kulinganisha na hapo awali.
Zana hizi zilileta maendeleo katika shughuli za kilimo na uwindaji.
Pia, zana hizi zilitumika kutengenezea nguo za asili za magome
ya miti na ngozi za wanyama. Magome ya miti yalipondwa na
mawe ili kulainishwa hadi kupata nguo.
Uthibitisho wa maendeleo ya sayansi na teknolojia za asili
katika utengenezaji na matumizi ya zana hizo kipindi cha Zama
za Mawe za Mwisho, unahusishwa na uwapo wa mabaki ya
zana kama mawe ya kusagia nafaka, mitego ya wanyama
na mabaki ya mifupa mikubwa ya wanyama kama tembo na
twiga katika mapango walimoishi binadamu wa kipindi hicho.
Inasadikiwa kwamba wanyama hao waliwindwa kwa kutumia
zana zilizotumika katika kipindi hicho.
Mchango wa sayansi na teknolojia asilia za Zama za Mawe
Zana za mawe zilileta maendeleo kadhaa katika maisha ya
48
06/11/2024 11:29:52
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 48
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 48 06/11/2024 11:29:52