Page 57 - Historiayatznamaadili
P. 57

Jedwali la 1, linaonesha hatua alizopitia binadamu katika Zama za Mawe.

              Jedwali la 1: Hatua alizopitia binadamu katika Zama za mawe

               Zama za Mawe za Kale          Zama za Mawe za Kati        Zama za Mawe za
          FOR ONLINE READING ONLY
                                                                         Mwisho
               1.  Binadamu aliishi kwa      1.  Binadamu alianza         1. Binadamu
                   kuchimba mizizi kwa           kutengeneza zana            alitengeneza zana
                   mikono, kuokota               za mawe za aina             za mawe bora
                   matunda na kutafuta           nyingi na bora zaidi        zaidi na nyepesi,
                   wadudu. Pia, aliishi          kulinganisha na zile        za aina nyingi
                   kwa kuwinda ndege,            za Zama za Mawe             na kwa matumizi
                   wanyama na kuokota            za Kale.                    mahususi.
                   mayai na mizoga.
                                             2.  Ugunduzi na              2. Wasanii na
               2.  Mwanzo wa historia ya         utengenezaji wa             mafundi walianza
                   sayansi na teknolojia         moto ulianza na             kutokea miongoni
                   za asili ya binadamu          uliwezesha binadmu          mwa wanajamii.
                   katika zama za mawe.          kula vyakula
                                                 vilivyochomwa, na        3. Binadamu
               3.  Ubunifu katika                kubanikwa. Pia,             alianzisha makazi
                   kutengeneza na                moto ulimsaidia             ya kudumu.
                   kutumia zana za mawe          kujihami dhidi ya           Pia, alianza
                   ulisaidia kuchimba            wanyama wakali na           mgawanyo
                   mizizi kwa mawe na            baridi kali.                wa kazi kwa
                   kuwinda wanyama na                                        kuzingatia jinsi,
                   ndege.                    3.  Binadamu aliweza            umri na uwezo wa
                                                 kuwinda wanyama             watu.
               4.  Maisha yalikuwa ya            zaidi. Pia, alianza
                   kuhamahama kwa ajili          kutengeneza              4. Binadamu
                   ya kutafuta chakula na        mavazi kwa kutumia          alianza kuwinda
                   makazi.  Hapakuwa             ngozi za wanyama            wanyama
                   na makazi ya kudumu.          zilizolainishwa.            wakubwa zaidi
                   Binadamu aliishi porini                                   kwa mishale
                   na mabondeni, karibu      4.  Binadamu alianza            ya sumu na
                   na mito akijitafutia          kuishi katika               kulima mazao ya
                   chakula.                      mapango.                    chakula.







                                                   50




                                                                                          06/11/2024   11:29:52
     Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd   50                                     06/11/2024   11:29:52
     Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd   50
   52   53   54   55   56   57   58   59   60   61   62