Page 60 - Historiayatznamaadili
P. 60
kuwinda na kujilinda dhidi ya wanyama wakali na maadui.
Zana zingine za chuma ni mundu, ambayo ilitumika kwa ajili ya
kufyeka na kusafisha maeneo kwa ajili ya kilimo. Vilevile, chuma
kilitumika kutengenezea visu kwa ajili ya kuchunia wanyama na
FOR ONLINE READING ONLY
kukatia nyama. Majembe yalitumika kulimia na kuchimbia mizizi
na wanyama wafukuao ardhi.
Baadhi ya zana za chuma ziliwekewa mipini ili kurahisisha
matumizi yake. Zana za chuma zilileta mapinduzi makubwa
katika sayansi na teknolojia asilia hasa katika kilimo, uwindaji,
ulinzi na uvuvi kabla ya ukoloni. Kielelezo namba 9, kinaonesha
zana za chuma zenye mpini.
Kielelezo namba 9: Zana za chuma zilizowekwa mpini
Baadhi ya jamii zilizojishughulisha na uzalishaji wa chuma ni
Wanyambo, Wahaya, Wazinza, Wafipa, Wapare, Wasambaa,
Wayao, Wangoni, Wahehe, Warongo na Wanyamwezi.
Kazi ya kufanya namba 3
Onesha katika ramani maeneo yalipo makabila
yaliyojishughulisha na ufuaji wa chuma.
53
06/11/2024 11:29:54
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 53
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 53 06/11/2024 11:29:54