Page 65 - Historiayatznamaadili
P. 65
hawakuruhusiwa kulima katika maeneo yenye vyanzo vya maji
na katika mifereji. Maeneo yaliyofanya kilimo cha umwagiliaji,
palikuwapo na kanuni za kutumia maji kwa ajili ya umwagiliaji.
Kwa mfano, watu waliruhusiwa kutiririsha maji katika mashamba
FOR ONLINE READING ONLY
yao kwa zamu. Pia, maji haya yalitumika kipindi cha ukame
tu. Hii ilifanyika kwa lengo la kuwezesha uhifadhi wa maji na
mgawanyo wa maji kwa watu wote. Pia, kilimo cha mazao
mchanganyiko kilifanyika ili kuhifadhi ardhi isichoke haraka.
Maadili haya yalisaidia uhifadhi wa ardhi na kuwa na maji kwa
ajili ya kilimo kipindi cha ukame. Sayansi na teknolojia hizo
zilisaidia kuongeza mazao ya kilimo.
Kazi ya kufanya namba 6
Jadili mambo uliyojifunza kuhusu maadili katika
sayansi na teknolojia za kilimo na jinsi ya
kuziendeleza katika kilimo kwa sasa.
Zoezi namba 2
1. Andika sayansi na teknolojia za asili katika kilimo
zilizotumika nchini kabla ya ukoloni.
2. Eleza maadili yaliyoambatana na shughuli za kilimo
kabla ya ukoloni.
3. Eleza umuhimu wa kutumia teknolojia asilia za kilimo
na maadili yake kwa jamii zetu kwa sasa.
Sayansi na teknolojia asilia katika ufugaji
Kazi ya kufanya namba 7
Fanya uchunguzi kuhusu shughuli za ufugaji
zinazofanyika katika maeneo yanayokuzunguka.
58
06/11/2024 11:29:55
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 58 06/11/2024 11:29:55
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 58