Page 67 - Historiayatznamaadili
P. 67
Kazi ya kufanya namba 8
Andika mambo uliyojifunza kuhusu sayansi na
teknolojia ya ufugaji na jinsi ya kuyaendeleza kwa
sasa.
FOR ONLINE READING ONLY
Sayansi na teknolojia za asili katika uvuvi
Sayansi na teknolojia asilia katika uvuvi ilitumia vifaa kama vile
ndoano, ngalawa, mitumbwi na mitego ya asili. Ndoano hizo
zilitengenezwa na jamii za wahunzi kwa kutumia chuma. Wavuvi
waliweka chambo mbalimbali katika ndoano ili kuvutia samaki
kwa lengo la kuwatega. Wavuvi waliweza kuwavua samaki
pindi walipokula chambo kwenye ndoano. Kielelezo namba 12,
kinaonesha uvuvi kwa kutumia ndoano.
Kielelezo namba 12: Uvuvi kwa kutumia ndoano
Pia, uvuvi ulifanyika kwa kutumia nyavu za asili zilizosukwa.
Wavuvi walitupa nyavu katika kina kirefu cha maji mengi ili
kuvua samaki. Samaki walipopita katika eneo walilotupa nyavu
walinaswa. Matumizi ya ngalawa na mitumbwi yalisaidia wavuvi
60
06/11/2024 11:29:56
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 60
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 60 06/11/2024 11:29:56