Page 68 - Historiayatznamaadili
P. 68
kwenda mbali kwenye maji yenye kina kirefu. Kielelezo namba
13, kinaonesha uvuvi kwa kutumia nyavu.
FOR ONLINE READING ONLY
Kielelezo namba 13: Uvuvi kwa kutumia nyavu
Vilevile, wavuvi walitumia mitego ya samaki kama vile madema
ambayo yalitokana na sayansi na teknolojia ya ususi. Sayansi
na teknolojia hizi ziliwawezesha wavuvi kuvua samaki wengi.
Uhifadhi wa samaki ulifanywa kwa kutumia chumvi na moto. Hii
ilisaidia kuwa na samaki kwa matumizi ya baadaye na kwa ajili
ya biashara.
Shughuli za uvuvi zilifanyika zaidi na jamii zilizoishi maeneo ya
maziwa, mito na katika sehemu za Pwani ya Bahari ya Hindi.
Jamii zilizoishi maeneo ya mwambao wa bahari na ziwa, ndizo
zilizojishughulisha zaidi na uvuvi. Mfano katika Pwani ya Bahari
ya Hindi na Visiwa vya Zanzibar, jamii zilizojihusisha na uvuvi
ni Wamakua, Wadigo, Watumbatu, Wandengereko, Wamwera
na Wakojani. Ukanda wa Ziwa Viktoria walikuwa Wakerewe,
Wajita, Wasukuma, Wakwaya, Wakara na Wajaluo. Ukanda
wa Ziwa Tanganyika ni Waha, na ukanda wa Ziwa Nyasa ni
Wanyasa na Wakisi.
61
06/11/2024 11:29:57
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 61
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 61 06/11/2024 11:29:57