Page 64 - Historiayatznamaadili
P. 64
kisha kuzifunika nyasi hizo kwa udongo ili kutengeneza tuta.
Mazao yalipandwa katika matuta. Sayansi na teknolojia hii
ilisaidia kuzuia mmomonyoko wa udongo wakati wa mvua.
Pia, maji yaliyokingwa katikati ya matuta yalitumika kuiweka
FOR ONLINE READING ONLY
ardhi katika hali ya unyevu kwa muda mrefu. Aina hii ya kilimo
iliwezesha ardhi iliyopo maeneo ya milimani na miinuko kutumika
kwa kilimo. Kielelezo namba 11, kinaonesha kilimo cha ngoro.
Kielelezo namba 11: Kilimo cha ngoro
Kazi ya kufanya namba 5
Chunguza na andika uwepo wa sayansi na teknolojia
za asili zilizotumiwa katika kilimo katika maeneo
yanayokuzunguka.
Maadili katika sayansi na teknolojia asilia katika kilimo
Maadili ilikuwa sehemu ya sayansi na teknolojia ya asili
katika kilimo. Mfano, jamii zilifanya kilimo cha msimu na cha
kuhamahama hasa maeneo yenye mvua chache. Maeneo
yenye mvua kubwa na rutuba kama vile, kando kando ya milima,
mito na kwenye mabonde kilifanyika kilimo cha kudumu. Watu
57
06/11/2024 11:29:54
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 57
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 57 06/11/2024 11:29:54