Page 62 - Historiayatznamaadili
P. 62
ni utengenezaji wa zana za chuma. Kimsingi zana za chuma
zilisaidia kurahisisha shughuli kama vile uvuvi, kilimo, uwindaji
na shughuli nyingine za uzalishaji mali katika jamii.
Kazi ya kufanya namba 4
FOR ONLINE READING ONLY
Jadili namna ya kuendeleza sayansi na teknolojia
ya ufuaji wa chuma kwa sasa.
Sayansi na teknolojia asilia katika kilimo
Kilimo ni mojawapo ya shughuli za kale iliyofanywa na jamii
nyingi za Tanzania kabla ya ukoloni.
Kilimo kwa kutumia zana asilia
Sayansi na teknolojia katika kilimo awali ilifanyika kwa kutumia
mawe na vijiti ili kuchimba na kufukua ardhi kwa lengo la kupanda
mbegu. Mabaki ya majivu yalitumika kama mbolea. Sayansi na
teknolojia hii ilikuwapo wakati wa Zama za Mawe za Mwisho;
binadamu alipoanza kutumia zana za mawe kwa ajili ya kulimia.
Aidha, sayansi na teknolojia za kilimo zilibadilika katika kipindi
cha ugunduzi wa chuma, kutokana na kuanza kutumika kwa zana
za chuma kama vile majembe, mapanga, mashoka na mundu
katika kilimo. Kipindi hicho, majembe yalitumika kuchimba na
kufukua ardhi kwa ajili ya kilimo. Mapanga, mashoka na mundu
vilitumika kufyeka majani, kukata miti ili kutayarisha shamba
kwa ajili ya kilimo.
Kilimo asilia cha umwagiliaji
Vilevile, sayansi na teknolojia asilia ya umwagiliaji ilitumika katika
shughuli za kilimo. Umwagiliaji ulifanyika kwa kuhifadhi maji
kwenye mabwawa yaliyojengewa kingo kwa mawe wakati wa
mvua za msimu. Kielelezo namba 10, kinaonesha mfano wa
bwawa lililojengewa kingo za mawe kwa ajili ya kuhifadhi maji
ya umwagiliaji.
55
06/11/2024 11:29:54
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 55
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 55 06/11/2024 11:29:54