Page 63 - Historiayatznamaadili
P. 63
FOR ONLINE READING ONLY
Kielelezo namba 10: Bwawa lililojengewa ukingo wa mawe
Maji yaliyohifadhiwa katika bwawa yalitumika kwa umwagiliaji
kipindi cha ukame. Watu hawakuruhusiwa kutumia maji haya
wakati wa mvua. Hii ilisaidia jamii kupata mazao muda wote.
Sayansi na teknolojia hii ilifanyika maeneo ya Engaruka,
Kaskazini mwa Tanzania katika jamii za Wairaqw. Pia, jamii ya
Wasonjo ilitumia sayansi na teknolojia hii.
Pia, baadhi ya jamii zilifanya umwagiliaji kwa kutumia mifereji
asilia ya kuchimba. Mifereji hii ilitoka katika vyanzo vya maji,
hasa katika maporomoko ya maji na milima na kutiririsha maji
hadi maeneo ya mashamba. Jamii zilizotumia teknolojia hii ni
Wapare na Wachaga.
Kilimo asilia kwa kutumia matuta
Maeneo yenye miinuko na mmomonyoko wa udongo, watu
walilima kwa kutumia matuta ya kukingama. Jamii kama vile
Wamatengo walitumia kilimo cha “ngoro”. Kilimo hiki kilifanyika
katika maeneo yenye mteremko ili kuzuia mmonyoko wa udongo
na kuiweka ardhi katika hali ya unyevunyevu. Kilimo cha ngoro
kilifanyika kwa kutandika nyasi katikati kwa umbo la mstatili,
56
06/11/2024 11:29:54
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 56
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 56 06/11/2024 11:29:54