Page 58 - Historiayatznamaadili
P. 58
Sayansi na teknolojia asilia za Zama za Chuma
Sayansi na teknolojia asilia za Zama za Chuma zilihusika katika
kutengeneza zana mbalimbali za chuma. Chuma kilipatikana
kwa kuchimba udongo (mbale) wenye chembechembe za madini
FOR ONLINE READING ONLY
ya chuma, kisha kuwekwa kwenye tanuru la moto mkali wa mkaa
ili kuuyeyusha. Sayansi na teknolojia hii ilisababisha madini ya
chuma yaliyochanganyikana na udongo kujitenga na kupata
majimaji ya chuma yaliyoganda katikati ya tanuru, mfano wa
mafukuto ya chuma safi yaliyoitwa kitali. Kitali kilitumika katika
kutengeneza zana za chuma. Kielelezo namba 6, kinaonesha
sayansi na teknolojia za ufuaji wa chuma.
Kielelezo namba 6: Sayansi na teknolojia ya ufuaji chuma
Kazi ya utengenezaji zana za chuma ilifanywa na wahunzi.
Zana za chuma zilitengenezwa kwa kutumia nyundo na mawe ili
kupata umbo husika. Moto ulitumika kuyeyusha chuma wakati wa
utengenezaji wa zana. Kielelezo namba 7, kinaonesha shughuli
za utengenezaji wa zana za chuma.
51
06/11/2024 11:29:53
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 51 06/11/2024 11:29:53
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 51