Page 54 - Historiayatznamaadili
P. 54
Kijiti cha kuchochea moto kilijulikana kama “ulindi” na
kilichopekechwa kilijulikana kama “ulimbombo”. Sayansi na
teknolojia ya utengenezaji wa moto ilileta maendeleo makubwa
katika maisha ya binadamu. Binadamu alianza kula chakula
FOR ONLINE READING ONLY
kilichopikwa, kubanikwa au kuchomwa, badala ya kula vyakula
vibichi kama ilivyokuwa hapo awali. Pia, matumizi ya moto
yalimsaidia binadamu kujihami na wanyama wakali. Mfano,
binadamu alitumia moto kuchoma majani ili kufukuza wanyama
wakali na kusaka wanyama wakati wa uwindaji. Vilevile, moto
ulimwezesha binadamu kupata mwanga na kuongeza joto ndani
ya mapango alimoishi. Aidha, sayansi na teknolojia ya asili ya
kutengeneza moto iliboresha utengenezaji wa zana za mawe.
Moto ulitumika katika kutengenezea gundi iliyotumika katika
uvishaji wa vichwa vya mishale na mikuki kwenye mipini. Zana
hizi ziliboresha shughuli za uwindaji.
Zoezi namba 1
1. Eleza maendeleo yaliyotokana na sayansi na teknolojia
wakati wa Zama za Kati za Mawe.
2. Eleza maendeleo yaliyopatikana kipindi cha ugunduzi
wa sayansi na teknolojia ya kutengeneza moto.
Zama za Mawe za Mwisho
Sayansi na teknolojia katika kipindi cha Zama za Mawe za
Mwisho ilikuwa na ubunifu zaidi ikilinganishwa na Zama za
Mawe za Kale na za Kati. Zana za Mawe za Zama za Mwisho
zilikuwa bora na nyepesi zaidi. Katika kipindi hiki binadamu
alitumia mawe kutengenezea mikuki, ncha za mishale na visu
vikali vyenye kuvutia zaidi. Pia, aligundua matumizi ya sumu
iliyotumika kwenye mishale. Kielelezo namba 5, kinaonesha
baadhi ya zana za mawe zilizotengenezwa kipindi cha Zama
za Mawe za Mwisho.
47
06/11/2024 11:29:51
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 47 06/11/2024 11:29:51
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 47