Page 51 - Historiayatznamaadili
P. 51
FOR ONLINE READING ONLY
Kielelezo namba 1: Utengenezaji wa zana, Zama za Mawe za Kale
Zana hizi zilimsaidia mwanadamu kuongeza mawindo na
chakula zaidi, kwani aliweza kuchimba mizizi mingi zaidi kwa
muda mfupi na kuua wanyama wadogo kwa ajili ya kitoweo.
Pia, zana hizo zilimsaidia kujihami na wanyama wakali. Vilevile,
zilitumika kuchunia ngozi za wanyama na kukata nyama. Aidha,
mawe yenye ncha kali yalitumika kukatia mizizi iliyotumika
kama chakula na dawa. Pia, yalitumika kutenganisha mizoga
ya wanyama ili kuwa rahisi kuibeba. Sayansi na teknolojia za
utengenezaji wa zana za mawe zilileta maendeleo makubwa
katika maisha ya binadamu kulingana na mahitaji ya jamii ya
wakati huo. Kielelezo namba 2, kinaonesha maumbo ya baadhi
ya zana za Zama za Mawe za Kale.
44
06/11/2024 11:29:50
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 44
Historia ya Tanzania na Maadili STD IV.indd 44 06/11/2024 11:29:50